MEZA YA FUTARI
Maghrib ilipofika, meza ya kufuturu ikajaa wapambe.
SAMBUSA alivyo mzuriiii…. akatongozwa na BW MKATE WA TAMBI. Kina MATOBOSHA wakamzoma “woooo umemkosaaa!!!” “BW.KEBAB ashamposaaa!!!”
Akaanza kulia kusikia kuwa sambusa keshachukuliwa.
VIAZI VYA MADONGE akamwambia, “na harusi itafanywa kwa khalle BHAJIA, siku ya IDD mungu akitujaalia.”
Salamu zikamfikia MKATE WA SINIA. ..Akamhurumia, akamwambia, “Swahib. acha kulia. “Penye nia hapakosi njia. “Kama ni wazuri, kila mahali wameenea”!! “Ukitaka, nitazungumza na hababa KIBIBI, akuozeshe jirani yake aitwae JELEBI.”
Hababa KIBIBI akaruka…”LA! Muhindi yule atamtesa, kweli ni mzuri, lakini apenda pesa. “Kwanini tusimuozeshe jamaa yetu KAIMATI?” Maskini mpaka sasa hajapata bahati.”Na ikiwa atakubali, mimi nitampelekea posa, kwa shangazi yake Bi.KILOSA.”
BW.MKATE WA TAMBI akaoona, yanini hii taabu, yanini hii aibu? “afadhali nimuowe cousin yangu TAMBI ZA ZABIBU.”
TAMBI ZA MAPAPAYU akafurahishwa na hio choice, akaieneza hio story hapo mezani upesi. Akajisifu kuwa yeye ndiye atakaye isimamia hio harusi….”Tutangoja ya kina SAMBUSA ikipita, yetu tutaifanya baada ya sita.”
Mjombake bw.harusi aitwae SPAGHETTI akaamua kujitolea, Italian SUITE, BISCOTTI na CAKE ZA CHOCOLATIE.”
KITUMBUA alipojua akasema..”Poleni, sitoiwahi hio harusi vile mimi ni mja mzito, lakini nawaahidi keshani nitajitolea SODA ZA VIMTO.”
MSETO akasema kwa majuto. “Natamani na mimi usiku wa kesha nijitolee WALI WA POJO, lakini watu washazowea MAHAMRI na VIAZI VYA ROJO.”
”Ikiwa hio harusi mutaipanga kwa mpango.” Akaruka nyanya TANGO. Mimi siku ya lunch nitajitolea juice ya MANGO.”
Akaanza kujisifu tajiri wa bw.harusi aitwae MBOGA ZA KIBANIANI. “Hapana tia wasiwasi….Mimi kutatoaa sufuria kumi za BIRIYANI.
Mchuzi wa KAMBA alitambaa aliposema atajitolea hall la kupamba.
SPRINGROLLS nae akasema ” basi na mimi najitolea kumpaka mkeo henna, na design nitakayomchora ni ya kichina.
Huku na huku, habari zikamfikia councillor KUKU. “Ikiwa watanialika, nitajitolea CHICKEN TIKKA. ”Wacha niwatie family ya kina sambusa homa, wakisikia napeleka mapaja ya kuchoma!”
Jamaa wakawa wana hamu akodishwe NDIZI ZA TAMU. Mwimbaji mzuri atokae huko Lamu. “Ikiwa atakosekana..mkodisheni VIAZI YA TAMU!!akatoa wasia ICE-CREAMU.
Aunty LASAGNIA akasema “wala Lunch yetu musikateni vitambara vya border, FALUDA atawauuzia sare rangi ya Powder.
CUTLESSI alivyo msabasi, akaanza kusengenya na MIKIA YA NGISI.
“Hmmm…si ajabu CHAPATI akatuvalia buibui, maana kila harus arepeat kanzu ile ile ya chuichui.”Na si ajabu wasialikwe kina ugali na mihogo,kwa umaskini wao na tabia zao za kidigo.
HA! HA! HA! akacheka SAMAKI WA KUPAKA.
‘Kweli yule chapati kanzu zake utafkiri zina viraka.Kama ni mimi mutanichoka! Nguo zangu zatoka America.”
“Kweeenda zakoooo!! Akamsutaaa…. MKATE WA UFUTA!! “Naskia wewe, MBAAZI na VIAZI VYA NAZI, fundi wenu ni TUI la NAZI.
“Nyote mumeshindwa na mpiga ramli bi. Mkia wa pweza. Mganga yule anavyo vaa dhahabu, abadan hamutomuweza.”
Wazee wa mji kina KAHAWA wakasema “Mupende musipende”. Kadhi tutakae waletea ni sheikh TENDE. “Kama ni shariff HALUWA ,amekabidhiwa UBALOZI! Na tangu aongezwe mshahara wa LOZI, siku hizi atutilia pozi.”
“Wacheni upuuzi !!!” Akawakemea NYAMA YA MBUZI.” Tena nyamazeni ! Hamjui kua leo ni RAMADHANI ? Hamuusikiii huo mwadhini? Mbona mwajitia madhambini?’ Twendeni tukaswalini, tusitokeni msikitini.” Kwani hamuoni, mpaka kesho jioni … sote tutakufa tuishie matumboniiii????
MORAL OF THE STORY
We are so engrossed with worldly pleasures and material life hence forget that we are on this earth to perfom Allah’s duties and obligations. When at the end of it all, we are all going to die and leave everything behind.

very interesting poem
By: nadya on August 28, 2010
at 3:50 pm
mashairi ya furahisha yafungua nafs.
tuma mashairi zaidi kama haya
By: ahmed mbark on August 29, 2010
at 4:07 pm
lol janami.. ilikuwa ni shairi la chakula, sifa za meza inavyo pambwa ramadhani, sifa na majina ya mapochopocho ama upishi bora wa chakula cha ramadhan…lol doesn’t matter shairi LIMENIBAMBA… NACHEKA PEKEYANGU …. KWA VYAKULA VILIVYO PAMBWA…. I WOULD LOVE TO HEAR SOME MASHAIRI IF UNAYO YALIYO SALIA,,,,
By: amore on May 24, 2011
at 12:29 am